Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba, Jumatano Septemba 6 2023, amempokea ofisini kwake Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Benki ya Dunia, anayesimamia ukuaji wa uchumi wenye usawa, fedha na taasisi zinazosimamia masuala ya fedha (EFI) katika ukanda wa Afrika, Bw. Hassan Zaman, ambapo wamejadili masuala mbalimbali ya uchumi na fedha.
Aidha, kikao hicho kilijadili ushirikiano kati ya Benki ya Dunia na Tanzania kwenye masuala ya uchumi kwa lengo la kuimarisha na kutatua changamoto za kiuchumi nchini.
Hii ni sehemu ya ziara ya kikazi ya Bw. Zaman, ambaye alipanga kukutana na Waziri wa Fedha, Governor wa BoT na viongozi wengine wa serikali kwa lengo la kudumisha ushirikiano kati ya pande zote mbili katika kukuza uchumi nchini.