Dhima yetu
Kudumisha utulivu wa bei na uadilifu katika sekta ya fedha kwa ukuaji jumuishi wa uchumi
Kudumisha utulivu wa bei na uadilifu katika sekta ya fedha kwa ukuaji jumuishi wa uchumi
Kuwa msimamizi anayehakikisha utulivu wa uchumi na mfumo wa kisasa wa kifedhaili kuendelea kuimarisha nchi katika ngazi ya uchumi wa kati na zaidi
Uadilifu:
Tunatekeleza majukumu yetu kwa uadilifu unaojionesha katika uaminifu, utii, ukweli na usiri.
Utendaji wa Mfano:
Tunatimiza wajibu wetu kwa umahiri na ubunifu ili kuboresha ufanisi wa shirika.
Uwajibikaji
Tunawajibika binafsi na kwa pamoja katika kutekeleza majukumu yetu.
Uwazi:
Tunatekeleza majukumu yetu kwa usahihi, uwazi na kuwasilisha taarifa muhimu kwa wadau wetu.
Ushirikishwaji:
Tunathamini ushirikishwaji mpana, utendaji kazi wa pamoja na kubadilishana ujuzi na uzoefu katika kutekeleza majukumu yetu.