Malengo na Majukumu
Malengo
- Kuchochea sekta jumuishi ya fedha inayowezesha utekelezaji Madhubuti wa sera ya fedha, uthabiti na imani kenye sekta ya fedha
- Kuimarisha imani na uhakika wa walaji katika matumizi ya bidhaa na huduma za fedha
- Kuchochea ukuaji wa teknolojia ya fedha na ubunifu unaochochea huduma jumuishi za kifedha kwenye sekta ya fedha
- Kukuza maendeleo ya sekta ya fedha kupitia ongezeko la ustawi katika upatikanaji wa mikopo na upanuzi wa huduma mbalimbali za kifedha
Majukumu
- Kufanya kazi za Sekretarieti kwenye shughuli za huduma jumuishi za kifedha
- Kuratibu wadau wa nchini, wa kikanda na wakimataifa kwenye masuala yanayohusiana na huduma jumuishi za kifedha na ustawi
- Kuendesha shughuli za majaribio ya ubunifu wa teknolojia ya fedha
- Kufanya tafiti kwenye masuala ya huduma jumuishi za kifedha
- Kupokea na kutatua malalamiko ya walaji wa huduma za kifedha
- Kufanya usimamizi wa mwenendo wa sekta ya fedha
- Kutekeleza mikakati ya kutoa elimu ya fedha
- Kusimamia utoaji wa dhamana kwa niaba ya Serikali