English | Mwanzo | Wasiliana nasi | Mrejesho | Tafuta
Nembo ya Serikali Benki kuu ya Tanzania Bank of Tanzania Logo
 
 

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

 
 
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
 
Nini Maana ya Mifumo ya Malipo ya Taifa?
Nani wadau wa Mifumo ya malipo ya Taifa Tanzania?
Njia zipi zilizozoeleka za malipo Tanzania?
Nini jukumu la Benki Kuu ya Tanzania katika Mifumo ya Malipo ya Taifa?
Rudi Mwanzo-NPS
 1. Nini Maana ya Mifumo ya Malipo ya Taifa?


  Mifumo ya malipo ya Taifa ni kundi la taasisi, vyombo na taratibu zinazotumika kuhakikisha mzunguko wa fedha nchini. Mifumo ya malipo ya Taifa inasaidia wigo mpana wa shughuli za kifedha kutoka katika biashara za kitanzania zinazofanyika ulimwenguni katika masoko ya kimataifa na pia katika kutoa huduma kwa mahitaji ya mtu mmoja mmoja kwa umma wa Tanzania.
 2. Nani wadau wa Mifumo ya malipo ya Taifa Tanzania?


  Wadau ni wote wenye maslahi katika Mifumo ya malipo ya Taifa. Hii inajumuisha wale wanamiliki, wanaotoa, wanoongoza au kutumia sehemu ya mfumo, au wanaochkua jukumu hilo. Wadau wakuu ni:-
  • Benki Kuu ya Tanzania; kama mamlaka ya kifedha Tanzania, inatimiza lengo katika uchumi na zaidi katika Mifumo ya malipo ya Taifa

  • Taasisi za Kifedha: benki za biashara na taasisi za kifedha zilizosajiliwa chini ya sheria ya Benki Kuu.

  • Watoaji wa Miundombinu, mfano kampuni za mawasiliano.

  • Watoa huduma za malipo, mfano SWIFT, waendeshasji wa malipo ya Kadi

  • Watumiaji wa mwisho wa Mifumo ya Malipo; mfano mtu mmoja mmoja, biashara za kampuni na serikali.

  • Mamlaka za udhibiti, mfano Soko la Hisa la Dar es Salaam, Mamlaka ya Soko la Mitaji na Dhamana.

  • Mamlaka za Kifedha za Kikanda na Mipango ya Kikanda; mfano Jumuiya ya Afrika Mashariki.

  • Mamlaka za Kifedha za Kimataifa; mfano IMF na Benki ya Dunia

 3. Njia zipi zilizozoeleka za malipo Tanzania?


  Fedha Taslimu: Hii ndio njia maarufu zaidi. Kwa ujumla inakubalika mahali popote kama fedha halali na hufaa zaidi kwa miamala yenye thamani ndogo. Kutokana na kupanuka kwa uchumi na maendeleo katika benki za kibiashara na Teknolojia ya habari na Mawasiliano, njia nyingine zisizo za fedha taslimu zimeanzishwa.
  • Paper-based instruments – these include payment orders, bills of exchange, promissory notes and cheques. Automated credit transfers and direct debits are included in this mode of payment.

  • Vyombo vya Karatasi - Hivi vinajumuaisha hati za malipo, bills of exchange, promissory notes na Hundi. Automated credit transfers and direct debits are included in this mode of payment.

  • Kadi za plastiki – zinajumuisha credit cards, debit cards, ATM na kadi za malipo ya baada.

  • Uhamishaji wa fedha kielektroniki – kutokana na matumizi ya TEHAMA, aina nyingi ya malipo kwa karatasi yamegeuka na kuwa katika mfumo wa kielektroniki, na zaidi katika miamala yenye thamani kubwa.

 4. Nini jukumu la Benki Kuu ya Tanzania katika Mifumo ya Malipo ya Taifa?


  Uendeshaji wa Mifumo ya Malipo kwa kiasi kikubwa una mahusiono na Malengo ya Benki Kuu ya Tanzania juu ya utulivu wa fedha. Majukumu ya Benki Kuu ya Tanzania ni pamoja na:
  • Kama mtumiaji wa Mifumo ya Malipo: Benki Kuu inayo miamala yake inayohitaji mzunguko wa fedha. Mfano malipo

  • Kama mshiriki wa Mifumo ya Malipo: Benki Kuu inaweza kutoa na kupokea malipo kwa niaba ya wateja wake kwa mfano Idara za Serikali na Benki Kuu nyingine.

  • Kama mtoaji wa Mifumo ya Malipo: utoaji wa akaunti za malipo kwa serikali na Benki za Biashara zinazoendeshwa katika mifumo ya malipo.

  • Kama Mlinzi wa Maslahi ya Umma: Jukumu hili ni pana na linajumuisha kati ya yafuatayo: Kuwa kama mdhibiti wa mifumo ya malipo, kuwa kama msimamizi washiriki wa mfumo, kutoa usimamizi na mipango ya mifumo ya malipo, kusuluhisha pale ambapo kutatokea malalamiko na kushughulikia taratibu za fidia.

  • Benki Kuu ya Tanzania inaweza pia kushirikishwa katika mambo kama vile kuchochea ushindani na ushirikiano na wakati huo ikihamasisha maendeleo na kupitishwa kwa viwango vya kiufundi.

  • Kama msimamizi wa Mifumo ya Malipo: Jukumu kuu la uangalizi la Benki Kuu ya Tanzania kimsingi limedhamiria kukuza utendaji makini wa mifumo ya malipo na kulinda mifumo ya kifedha dhidi ya “domino effects”.

 

| Bank of Tanzania Training Institute | Webmail Access | Deposit Insurance Board | Archive Directory | Jobs, Tenders and Press Release |

 
Site Map | Website Disclaimer | Privacy Policy | Email Disclaimer | Webmaster@bot.go.tz