English | Mwanzo | Wasiliana nasi | Mrejesho | Tafuta
Nembo ya Serikali Benki kuu ya Tanzania Bank of Tanzania Logo

Masoko ya Fedha

Masoko ya Fedha Tanzania

Masoko ya fedha nchini Tanzania yanahusisha hati fungani, masoko ya fedha za kigeni, na miradi ya pamoja ya uwekezaji. Benki Kuu ya Tanzania inalenga utekelezaji wa sera za fedha, kuhakikisha kuwa serikali inapohitaji ya fedha zinapatikana na kuwezesha utulivu na ufanisi wa masoko.

Hatua kubwa katika masoko ya fedha katika Tanzania

Masoko ya fedha ya Tanzania yanahusisha hati fungani, dhamana za Serikali, masoko ya fedha za kigeni (ya jumla na rejareja), dhamana za makampuni na hisa. Katika kutekeleza wajibu wake, Benki Kuu hutumia mfumo wa kuuza na kununua dhamana za muda mfupi kufikia malengo yake matatu ambayo ni kusimamia ujazo wa fedha, kujazia upungufu kwenye bajeti na kutoa kigezo kwa riba za mabenki.

Kuanzishwa kwa masoko ya fedha na mitaji (money and capital markets) kumeiwezesha Serikali kukopa katika mfumo wa moja kwa moja kutoka kwa umma ili kujazia upungufu kwenye bajeti. Hii ni tofauti na ilivyokuwa hapo awali wakati Serikali ilivyokuwa inakopa moja kwa moja kutoka Benki kuu. Ieleweke wazi kuwa, matumizi ya mfumo wa ukopaji usiosababisha mfumuko wa bei kupitia hati fungani na dhamana za Serikali, umechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza ziada ya fedha katika mzunguko.

Tumetoka mbali, wakati ambapo uuzaji wa hati fungani na dhamana za Serikali ulifanywa pasipo teknolojia (manually) na bila matumizi ya mfumo bora wa malipo (settlement system), ambapo wawekezaji walilazimika kubeba vikapu vya hela kufanya malipo Benki Kuu! Kipindi hicho kilihusisha utoaji wa hati za umiliki, na utumiaji wa masanduku kwa ajili ya kupokelea maombi (tender) ya uwekezaji katika hatifungani na dhamana za serikali.

Katika kukabiliana na hili na kuboresha mfumo huu wa ukopaji, mnamo mwaka 1999, Benki kuu iliona umuhimu wa kuanzisha mfumo ulio bora (computerised book entry system) wa uuzaji na utunzaji wa hatifungani na dhamana za serikali usiohusisha utoaji wa hati (physical certificates). Mfumo huo unahusisha utunzaji wa kumbukumbu, uhamishaji na uwekaji sawa (updating) wa umiliki wa dhamana na hatifungani. Mbali na hayo, mfumo huo pia una uwezo wa kugawanya hati fungani pamoja na dhamana za Serikali kukidhi matakwa ya mmiliki, hivyo kurahisisha uuzaji wake katika soko la upili. Manufaa mengine ya mfumo huu wa utunzaji wa umiliki wa dhamana hizi ni kama ifuatavyo:

  • Ni njia salama na rahisi ya umilikaji wa dhamana hizi ukilinganisha na mfumo wa umiliki kwa kutumia hati.
  • Inawezesha kuondokana na utozwaji wa ushuru unapobadilisha umiliki wa dhamana za Serikali
  • Inaongeza ufanisi katika ununuzi na uuzaji wa dhamana za Serikali
  • Ina rahisisha utoaji huduma za mikopo kati ya mabenki (Interbank cash market)
Mfumo huu umeendelea kuboreshwa mpaka leo hii tunazindua mfumo ulio bora zaidi, unaozingatia utaratibu bora na kanuni za kimataifa, ikiwa ni pamoja na kuhusisha mtandao katika muamala (online transaction features), jambo linalopelekea ufanisi katika mfumo mzima. Ni muhimu kutambua kwamba mfumo huu unaiweka Tanzania katika nafasi ya kwanza katika Afrika Mashariki kuwa na mfumo unaoruhusu muamala katika mtandao, katika soko la awali na soko la upili la hati fungani na dhamana za Serikali. Mategemeo yetu ni kuona ongezeko la ubora na ufanisi katika masoko ya hati fungani na dhamana za Serikali, jambo litakalopelekea kudhibiti athari hasi (risk) mikopo na masoko, pamoja na kuongeza muamala katika soko la upili.

Soko la fedha (money market)

Soko la fedha linajumuisha hati fungani(Tbill and Tbonds),mikataba ya kukopeshana pesa kwa kutumia hati fungani(Repo/Reverse Repo),kukopeshana baina ya mabenki(IBCM) na kuuziana pesa za kigeni.

Hati fungani(Tbill and bond)

washiriki wakuu ni benki za biashara na ushiriki mdogo wa wawekezaji wa ndani. Katika hati fungani za muda mfupi zinahusisha mnada wa siku 35,91,182 na 364 na hati fungani za muda mrefu zinaanza za miaka 2,5,7,10 na 15.kwa maelezo Zaidi bofya hapa

Mikataba ya kukopeshana baina ya mabenki (Repos/Reverse repo)

kuhusisha uuzaji wa dhamana kwa makubaliano ya kurudisha kwa baadae na katika bei waliyokubaliana na hili zoezi lina muda maalum kuanzia siku 2 mpaka 14. MRA_FINAL_Repurchase_Agreement.Sep2010
Mkopeshano baina ya mabenki (IBCM)hii inayapa mabenki nafasi ya kukopa na kukopesha na hii inawasaidia wakati wakiwa wana shida ya pesa kati yao wenyewe.

Soko la pesa za kigeni

Miamala yote ya pesa za kigeni inafanyika kati ya benki kuu na mabenki na pia wabenki ya biashara yenyewe kwa yenyewe na pia inahusisha wateja wa mabenki na maduka ya pesa za kigeni.kiwango kikubwa cha miamala ya pesa za kigeni kinafanyika kati benki kuu na mabenki ya biashara na hii ndiyo inayowezesha kiwango cha kubadilisha pesa kwa kila siku(exchange rates)

Soko la hisa la Dar es salaam

soko la hisa la Dar es salaam ni mmoja wa washiriki katika soko la fedha Tanzania ambapo kazi kubwa ya wanayofanya ni kutafuta mitaji ya makampuni mbali mbali ambayo yatakuwa wameyasajili kwenye soko la hisa na pia ndiyo sehemu ambayo soko la upili linafanyika kwa maelezo Zaidi bofya hapa
http://www.dse.co.tz

Soko la mitaji na dhamana Tanzania

Hii taasisi ni moja wapo inahusika na masoko ya pesa nchini ambapo majukumu yake makubwa ni pamoja Kukuza na kuendeleza ufanisi masoko ya mitaji na dhamana ya biashara katika Tanzania wakati kuhakikisha shughuli inakuwa endelevu. Kuunda kanuni kwa ajili ya uongozi wa sekta hiyo, ulinzi wa maslahi ya wawekezaji na uadilifu wa dhamana soko dhidi ya ukiukwaji wowote; Kutoa Leseni na kusimamia masoko ya hisa, wafanyabiashara, mawakala na wawakilishi wao na washauri wa uwekezaji Kutoa ushauri kwa Serikali kuhusu sera na masuala yote yanayohusiana na sekta ya dhamana. Kujenga mazingira muhimu kwa ukuaji utaratibu na maendeleo ya soko la mitaji. 

| Chuo cha Benki Kuu | Webmail Access | Bodi ya Bima ya Amana | Kumbukumbu | Ajira, Zabuni, Taarifa kwa Umma |

 
Mpangilio wa Tovuti | Tahadhari kwenye Tovuti | Sera ya Faragha | Tahadhari kwenye barua pepe | Webmaster@bot.go.tz