English | Mwanzo | Wasiliana nasi | Mrejesho | Tafuta
Nembo ya Serikali Benki kuu ya Tanzania Bank of Tanzania Logo

Usimamizi wa Mabenki

Mbinu za Usimamizi

Benki kuu imepitisha mbinu ya usimamizi wa mabenki na Taasisi za Fedha unaozingatia vihatarishi (Risk Based Supervision). Mfumo uzingatiao vihatarishi unatoa utaratibu na muundo wa kutathimini aina mbali mbali za vihatarishi ilio wa kipekee kwa kila benki na taasisi ya fedha ambao huwezesha vihatarishi vyote huchambuliwa kwa ufanisi zaidi. Mfumo huu unaruhusu maamuzi juu ya uwezekano wa uwepo wa vihatarishi kwenye taasisi mbalimbali kutumia mizani sawa. Usimamizi unaozingatia vihatarishi unazingatia kuwa rasilimali ni chache na kwamba zina kikomo na hivyo inalenga kuzitumia rasilimali zilizopo katika njia ya ufanisi zaidi. Katika kufanikisha malengo ya Benki kuu ya kuhakikisha utulivu, usalama na uthabiti wa mfumo wa mabenki nchini, Benki inatumia njia mbili za ukaguzi/ufuatiliaji ambazo ni ule unaohusu kutembelea na kukagua nyaraka mbalimbali katika sehemu za kazi za taasisi husika (Onsite surveillance) na unaohusu kuchambua taarifa mbalimbali zinazowasilishwa Benki kuu na taasisi za fedha (offsite surveillance).

i. Mfumo unaohusu kutembelea na kukagua nyaraka mbalimbali katika sehemu za kazi za taasisi husika (Onsite surveillance)

Mfumo unaohusu kutembelea na kukagua nyaraka mbalimbali katika sehemu za kazi za taasisi husika unajumuisha uchunguzi wa wigo mpana (full scope examination) na uchunguzi uliolenga sehemu maalumu (Targeted onsite examination). Mapitio ya mfumo wa usimamizi wa vihatarishi wa kila benki au taasisi ya fedha hufanywa na huzingatia vihatarishi vifuatavyo; mikopo, ukwasi, masoko, ufuataji sheria, mkakati na uendeshaji. Licha ya Mapitio ya mfumo wa usimamizi wa vihatarishi, pia upitiaji wa vitu muhimu vifuatavyo hufanywa, utoshelezaji wa mtaji, ubora wa rasilimali, ubora wa usimamizi, uwezo wa kupata mapato, usimamizi wa ukwasi na uhisia wa vihatarishi vya soko (Capital adequacy, Asset quality, Management quality, Earnings capability, Liquidity and Sensitivity to market risk). Zaidi ya hayo, wakaguzi hutathimini ufanisi wa mfumo wa udhibiti wa ndani wa benki au taasisi ya fedha wanzazozikagua.

ii. Mfumo unaohusu kuchambua taarifa mbalimbali zinazowasilishwa Benki kuu na taasisi za fedha (offsite surveillance).

Mfumu huu hutathimini uthabiti wa kifedha kwa kuchambua takwimu na nyaraka zinginezo zielezazo juu ya maeneo muhimu ya benki au taasisi ya fedha. Takwimu na ripoti hukusanya kila baada ya kipindi maalumu ( kila siku, kila wiki, kila baada ya wiki mbili, kila mwezi, kila robo mwaka, kila nusu mwaka au kila inapohitajika).

 

| Chuo cha Benki Kuu | Webmail Access | Bodi ya Bima ya Amana | Kumbukumbu | Ajira, Zabuni, Taarifa kwa Umma |

 
Mpangilio wa Tovuti | Tahadhari kwenye Tovuti | Sera ya Faragha | Tahadhari kwenye barua pepe | Webmaster@bot.go.tz