English | Mwanzo | Wasiliana nasi | Mrejesho | Tafuta
Nembo ya Serikali Benki kuu ya Tanzania Bank of Tanzania Logo

Usimamizi wa Benki

Maduka ya kubadilisha fedha

Kuna maduka ya kubadilisha fedha yapatayo 284 yanazoendesha shughuli zao nchini ana mbazo yamepewa leseni na Benki Kuu ya Tanzania.

Kuna aina mbili za maduka ya kubadilisha fedha za kigeni, yaani maduka ya Daraja A na yale ya Daraja B. Duka la daraja A linashughulika na miamala ya papo kwa papo ya kubadilisha fedha za kigeni na hati nyingine za malipo zilizoizinishwa, wakati duka la daraja B linashughulika na miamala ya papo kwa papo ya kubadilisha fedha za kigeni na hati nyingine za malipo zilizoizinishwa na biashara za utumaji fedha kama mawakala wadogo wa Mawakala wa Kimataifa wa utumaji Fedha au waendeshaji wa mitandao ya simu au shughuli nyingine kama zitakavyoidhinishwa na Benki Kuu. Kila daraja la maduka ya kubadilisha fedha yanahitaji mtaji tofauti ili kuanzishwa.
Benki kuu itatoa maamuzi ya kutoa au kutotoa leseni ya muda ndani ya siku thelathini (30) baada ya kupokea nyaraka zote zinazohitajika kutoka kwa mtu aombae kuruhusiwa kuanzisha duka la kubadilisha fedha. Yafuatayo ni mahitaji kwa ajili ya maombi ya kuanzisha maduka ya kubadilisha fedha.

  • Orodha ya mahitaji ya kuanzisha maduka ya kubadili fedha
  • Fomu ya maombi ya kuanzisha maduka ya kubadili fedha

 

| Chuo cha Benki Kuu | Webmail Access | Bodi ya Bima ya Amana | Kumbukumbu | Ajira, Zabuni, Taarifa kwa Umma |

 
Mpangilio wa Tovuti | Tahadhari kwenye Tovuti | Sera ya Faragha | Tahadhari kwenye barua pepe | Webmaster@bot.go.tz