English | Mwanzo | Wasiliana nasi | Mrejesho | Tafuta
Nembo ya Serikali Benki kuu ya Tanzania Bank of Tanzania Logo

Huduma za Kibenki

Idara ya Sarafu

Kwa mujibu wa Sheria ya Benki Kuu ya mwaka 2006, Benki Kuu ya Tanzania ni benki pekee yenye jukumu la uandaaji, usanifu, uagizaji na usambazaji wa noti na sarafu ambazo ni fedha halali kwa malipo ya Kitanzania. Kazi hizo hufanyika kwa kuangalia mahitaji ya taifa kwa ujumla ili kuhakikisha uwepo wa uwiano mzuri wa upatikanaji wa fedha kwa mchanganuo (denominations) na kiwango kinachohitajika.

Idara ya Sarafu ina jukumu la kuhakikisha kuwa Sera ya Fedha Safi (Clean money Policy) inatekelezwa na malengo yanafikiwa kwa kuhakikisha fedha (noti na sarafu) zinafika katika mikoa yote ya Tanzania kulingana na mahitaji. Benki Kuu inasambaza fedha kupitia matawi yake yaliyopo Arusha, Zanzibar, Dodoma, Mwanza, Mbeya na Mtwara. Pia ina jukumu la kutoa huduma za kuweka fedha kwa mabenki ya biashara na taasisi za fedha na kutoa elimu ya utambuzi wa noti halali na jinsi ya kutunza noti kwa jamii.

Pia Benki Kuu imefungua vituo maalum vya usambazaji fedha katika baadhi ya mikoa ambayo hakuna matawi ya Benki Kuu; vituo hivi huwa ndani ya mabenki ya biashara na kazi yake kuu ni kutoa huduma kwa wananchi ya usambazaji wa fedha kwa niaba ya Benki Kuu. Vituo hivyo viko katika miji ya Mtwara, Songea, Sumbawanga, Bukoba, Tabora, Kigoma, Tanga, Pemba na Shinyanga.

Wasiliana Nasi:

Ofisi za Idara ya Sarafu zipo ghorofa ya Pili, Mnara wa Kaskazini; Jengo la Benki Kuu ya Tanzania, Mtaa wa 2 Mirambo, 11884 Dar es Salaam.

Mhandisi. G. N. Amon, Meneja
Idara ya Sarafu
Barua Pepe: GNAmon@bot.go.tz
Simu: +255 22 2235673

 

 

| Chuo cha Benki Kuu | Webmail Access | Bodi ya Bima ya Amana | Kumbukumbu | Ajira, Zabuni, Taarifa kwa Umma |

 
Mpangilio wa Tovuti | Tahadhari kwenye Tovuti | Sera ya Faragha | Tahadhari kwenye barua pepe | Webmaster@bot.go.tz