English | Mwanzo | Wasiliana nasi | Mrejesho | Tafuta
Nembo ya Serikali Benki kuu ya Tanzania Bank of Tanzania Logo

Idara ya Huduma za Kibenki

Idara ya Huduma za Kibenki ni sehemu ya Kurugenzi ya Huduma za Kibenki inayojishughulisha na utoaji Huduma za kibenki kwa Serikali Kuu za Tanzania, mabenki ya biashara na taasisi za fedha. Idara hii inahusika na utunzaji wa akaunti za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Miongoni mwa majukumu ya idara hii ni kufanya malipo, kupokea fedha kwa niaba ya serikali zilizotajwa hapo juu, kuhamisha fedha na kupokea na kutunza mapato ya serikali, pia kutunza akaunti za mabenki ya biashara na taasisi za fedha. Vile vile idara hii ina jukumu la. kusimamia kazi za ubadilishanaji hundi baina ya benki za biashara (Clearing House) na pia kuwezesha malipo ya Lombard facility kwa mabenki ya kibiashara. Pia inahusika na uchapishaji na usambazaji wa hundi zinazotumika na serikali na wizara zake.

 

 

Wasiliana Nasi:

Ofisi za Idara ya Huduma za Kibenki zipo ghorofa ya Kwanza, Mnara wa Kaskazini; Jengo la Benki Kuu ya Tanzania, Mtaa wa 2 Mirambo, 11884 Dar es Salaam.

Barua Pepe: info@bot.go.tz
Simu: +255 22 2235135

 
 

| Chuo cha Benki Kuu | Webmail Access | Bodi ya Bima ya Amana | Kumbukumbu | Ajira, Zabuni, Taarifa kwa Umma |

 
Mpangilio wa Tovuti | Tahadhari kwenye Tovuti | Sera ya Faragha | Tahadhari kwenye barua pepe | Webmaster@bot.go.tz