English | Mwanzo | Wasiliana nasi | Mrejesho | Tafuta
Nembo ya Serikali Benki kuu ya Tanzania Bank of Tanzania Logo

Kuhusu Benki Kuu

Historia ya Benki Kuu

Benki Kuu ya Tanzania ni Taasisi ya Umma ambayo ilianza kufanya kazi rasmi tarehe 14 Juni 1966 kwa mujibu wa Sheria ya Benki Kuu Na. 12 ya mwaka 1965. Sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho mwaka 1978. Aidha, mwaka 1995 ilitungwa sheria mpya ya Benki Kuu na kufanyiwa maboresho mwaka 2006 ili kutoa mamlaka zaidi kwa Benki Kuu katika kusimamia utekelezaji wa sera ya fedha.

JUKUMU LA MSINGI

Jukumu la msingi la Benki Kuu ya Tanzania ni kuandaa na kutekeleza sera ya fedha inayolenga kudhibiti mfumuko wa bei na kujenga mfumo wa fedha ulio imara na unaofaa kwa ukuaji endelevu wa uchumi wa taifa.

Kazi zingine za Benki Kuu:

 • Kutoa sarafu ya nchi ambayo ni Shilingi ya Tanzania
 • Kusimamia mabenki na taasisi za fedha
 • Kusimamia na kudhibiti mifumo ya malipo nchini
 • Kuhifadhi akiba ya nchi ikiwemo fedha za kigeni
 • Kutoa ushauri juu ya masuala ya uchumi na fedha kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
 • Benki ya Serikali, na
 • Benki ya Mabenki.

Dira Yetu
"Kuwa Benki Kuu ya mfano iliyojikita katika kudhibiti mfumuko wa bei na kujenga mfumo wa fedha ulio imara unaofaa kwa ukuaji endelevu wa uchumi wa taifa."

Dhima Yetu
"Kuandaa na kusimamia sera ya fedha inayolenga kudhibiti mfumuko wa bei na kujenga mfumo wa fedha imara na wenye uadilifu unaofaa katika kuleta ukuaji endelevu wa uchumi wa taifa."

Tunu

Ili kutimiza majukumu yake, Benki Kuu inazingatia Tunu zifuatazo:
"Uadilifu, Ushirikishwaji, Ufanisi na Uwajibikaji".

 1. Uadilifu: Tunazingatia na kujali maadili mema katika utendaji wetu wa kazi yanayojidhihirisha katika uaminifu, ukweli, kujituma na kutunza siri wakati wa utekelezaji wa majukumu yetu
 2. Ushirikishwaji: Tunaamini katika ushirikishwaji wa wafanyakazi wote, kufanya kazi kwa pamoja na kutumia umahiri na uzoefu tulio nao katika kutimiza malengo yetu.
 3. Ufanisi: Tunajali kufanikisha malengo yetu kwa weledi na ubunifu wa hali ya juu, na wakati wote tunajitahidi kuboresha utendaji kazi wa Taasisi.
 4. Uwajibikaji: Sote kwa pamoja na kila mmoja wetu tunawajibika kwa yote tunayotenda. Aidha, kwa juhudi na maarifa tunaahidi kukidhi haja na matarajio ya wadau wetu.

Jukumu la Msingi la Benki Kuu
 

 

| Chuo cha Benki Kuu | Webmail Access | Bodi ya Bima ya Amana | Kumbukumbu | Ajira, Zabuni, Taarifa kwa Umma |

 
Mpangilio wa Tovuti | Tahadhari kwenye Tovuti | Sera ya Faragha | Tahadhari kwenye barua pepe | Webmaster@bot.go.tz